Nuru FM

Mafinga wakamilisha ujenzi wa Miradi ya Boost.

26 July 2023, 7:36 pm

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego akizungumza baada ya kukagua miradi ya Boost. Picha na Idara ya Habari Mafinga Mji.

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego ameipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga kwa Utekelezaji wa Miradi ya BOOST.

Dendego ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea Shule ya Msingi Nyamalala iliyokamilisha ujenzi wa vyumba vitano(5) vya madarasa na matundu matatu(3) ya vyoo na Ujenzi wa vyumba sita(6) vya madarasa na matundu matatu(3) ya vyoo vya wanafunzi wasichana katika Shule ya Msingi Gangilonga.

Amesema lazima wanafunzi waambiwe ukweli kuhusu Mazingira wanayosomea kuwa ni mazuri kuna ujenzi wa Madarasa unaendelea, matundu ya vyoo na zaina za kufundishia zinatolewa na Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tofauti na miaka ya zamani ambapo Mazingira ya kusomea yalikuwa sio rafiki.

“Walimu watusaidie kuwaambia wanafunzi kule tulikotoka sisi hatukusoma madarasa mazuri hivi, yalikuwa Ni giza hayana hata umeme, kwahiyo kauli za wanafunzi kusema hakuna kitu kilichofanyika sio sawa , mabadiriko ni makubwa yanayofanywa na Serikali iliyo madarakani “ Mhe. Halima Dendego RC Iringa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufindi Ndugu Frank Sichalwe alipata fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Gangilonga ambayo inatekeleza ujenzi wa vyumba sita vya madarasa na matundu matatu ya vyoo.
Shule ilipokea kiasi cha shilingi 156,000,000/- kutoka Serikali Kuu. Ujenzi umekamilika.

Ziara ya Mkuu wa mkoa imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu, Ayoub Kambi pamoja na wakuu wa Divisheni na vitengo Halmashauri ya Mji Mafinga.