Nuru FM

Mbunge Midimu aibana serikali kujenga Daraja Simiyu

8 May 2023, 11:22 am

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Esther Midimu akiuliza Swali Bungeni Jijini Dodoma. Picha na Mwandishi wetu.

Na Mwandishi wetu

Serikali imetakiwa kujenga Daraja la Mto Duma- Bariadi lililopo Mkoani Simiyu ambalo limekuwa likijaa kipindi Cha Mvua.

Hayo yamezungumzwa Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi Cha maswali na majibu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu Esther Midimu na kuongeza kuwa ni vyema serikali ikawahakikishia wananchi ujenzi wake.

Katika Swali la Nyongeza Mh. Esther aliuliza kuwa serikali ina mpango Gani wa kujenga Daraja la Barabara inayounganisha Wilaya ya Itilima kwenda hospital ya Misheni.

Akijibu Swali hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEM Deogratius Ndejembi amesema kuwa katika kukidhi haja ya kuwa na mawasiliano kwa wananchi wanaotenganishwa na Mto huo, serikali imetenga jumla ya milioni 50 katika mwaka wa fedha 2023-2024 ili kufanya usanifu wa Daraja hilo.

Mh. Ndejembi Amesema kuwa eneo hilo Lina uhitaji wa madaraja mawili na tayari imeshaanza kujenga Daraja Moja katika Barabara ya Igugu, Matongo na Gibishi.

Hata hivyo Naibu Waziri TAMISEM amebainisha serikali inatekeleza kipaumbele chake kwa kushirikiana na Tarula kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora za Barabara.