Nuru FM

Watendaji wa Kata Mafinga Mji wakabidhiwa Pikipiki.

16 November 2023, 10:23 am

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge na Mkurugenzi wa Mafinga Mji wakikata Ayoub Kambi wakikata utepe.

Na Mwandishi Wetu.

Jumla ya pikipiki 7 zenye thamani ya shilingi 22,129,100/-zimekabidhiwa kwa watendaji wa Kata nne za pembezoni na wakusanya mapato Katika Halmashauri ya Mji Mafinga ili kuboresha utendaji kazi na ukusanyaji wa Mapato.

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi Ndugu Honest Mlambo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu Ayoub Kambi amesema pikipiki hizo ni kwaajili ya Watendaji wa Kata nne za Isalavanu, Sao Hill, Rungemba na Kinyanambo baada ya kutambua changamoto za watendaji wa Kata katika kuyafikia maeneo yao ya Kiutendaji pamoja na wakusanya mapato.

Amesema kuwa Ununuzi wa Pikipiki hizo ni kutokana na mapato ya ndani kwa bajeti ya mwaka wa Fedha 2022/2023.

Akikabidhi Pikipiki Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema lengo la kukabidhi vyombo hivyo vya usafiri Ni kuwawekea mazingira mazuri Watendaji na wakusanya Mapato katika Utekelezaji wa Majukumu yao.

Hafla hiyo umehudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Frank Sichalwe, Waheshimiwa Madiwani wa Kamati ya Fedha pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Mji Mafinga.