Mufindi wajiandaa kuupokea Mwenge
24 May 2026, 09:53

Mwenge huo utatembelea kata zote za Wilaya ya Mufindi DC na Halmahauri ya Mji Mafinga kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Na Fredrick Siwale
Wilaya ya Mufindi inatarajiwa kuupokea mwenge wa Uhuru tarehe 26/6/2026 ukitokea Mkoani Njombe kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Dkt. Linda Salekwa na kuongeza kuwa Mwenye huo utatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo Mapokezi yatakuwa katika shule ya Sekondari Malangali na Mkesha Kuwa Katika Shule Ya Sekondari Saadan.
Dkt Linda amesema kuwa Mwenge wa uhuru utakimbizwa katika kata tano za Halmashauri ya Mufindi DC na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa afya, elimu na Mazingira.
Aidha Linda amesema kuwa Miradi 7 yenye thamani ya Bilion 18 itazinduliwa na kuwekea jiwe la msingi Wilaya ya Mufindi DC huku Mafinga Mji wakitarajia kuupokea mwenge na kukimbizwa katika kata zote tano.
Aidha amewataka Wananchi Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kushiriki katika mapokezi ya Mwenge huo ambao utawaonesha utekekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.