Nuru FM

Wananchi walia ubovu wa barabara

18 May 2021, 8:44 am

Wananchi wa Ugele Ilangila na ugele Manyigi Kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa barabara jambo linalopelekea usafiri kukosekana katika eneo lao.Wakizungumza na Nuru fm baadhi ya wananchi wana mtaa huo wamesema kuwa changamoto ya barabara imekuwa ikisababisha waingie gharama kubwa wakitaka kwenda mjini kufuata huduma

Wakizungumza na Nuru fm baadhi ya wananchi wana mtaa huo wamesema kuwa changamoto ya barabara imekuwa ikisababisha waingie gharama kubwa wakitaka kwenda mjini kufuata huduma za kijamii.

Wananchi hao wamesema kuwa ubovu wa barabara umepelekea hata usafiri iwe tabu kwao kwani hakuna Basi ambalo linafanya safari zake katika kijiji chao.

Aidha wananchi hao wameiomba serikali kuwatatulia kero ya ubovu wa miundombinu kwani wanapata shida ya usafiri licha ya wao kulipa kodi kupitia mazao wanayolima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ugele Ilangila Bw. Valentino Vitus Mligo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akikiri kuwa Diwani wa Kata ya Mkimbizi akiwaahidi kutatua kero hiyo hiyo.

Naye Diwani wa kata ya Mkimbizi Eliudi Mvela amesema kuwa anatambua kero ya barabara na atawasiliana na TARULA kwa ajili ya kuanza kuikarabati.