Nuru FM

SAOHILL wapanda miti zaidi ya 2000

24 March 2024, 10:46 am

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa akikagua zoezi la upandaji miti. Picha na mwandishi wetu.

Kuhifadhi vyanzo vya maji kunaendana sambamba na zoezi la upandaji wa miti katika maeneo yanayotunguka.

Na Mwandishi wetu

ZAIDI ya vyanzo 20 vya maji vimehifadhiwa katika shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambavyo vimekuwa vikihudumia miradi mikubwa na midogo ya wilaya na kitaifa.

Akizungumza wakati wa upandaji miti katika kata ya Bumilahinga kijiji cha Ulole,Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti Saohill PCO Tebby Yoram alisema kuwa uongozi wa shamba la miti Sao Hill wamekuwa mstari wa mbele kuhifadhi vyanzo vya maji kwa manufaa ya taifa.

PCO Yoram aliwaomba wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadaye kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Lakini pia PCO Yoram alisema kuwa katika kuadhimisha siku ya upandaji miti shamba la miti Sao Hill walipanda zaidi ya miti 2000 rafiki na maji katika kata ya Bumilahinga kwa kuzunguka vyanzo vyote vya maji.