Nuru FM

Iringa watakiwa kutumia dawa kwa kufuata ushauri wa wataalam wa afya

24 April 2024, 10:14 am

Picha ya Mfano wa dawa zinazotumiwa na wananchi kwa ajili ya kutibu maradhi. Picha kwa msaada wa mtandao.

Kutofuata ushauri wa wataalamu wa afya katika matumizi ya dawa Husababisha magonjwa kama ugonjwa wa figo, Ini na usugu wa ugonjwa.

Na Joyce Buganda

Wananchi wa Manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia dawa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya ili kuepukana na madhara.

Hayo yamezungumzwa na Daktari wa magonjwa ya ndani kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa Dokta Ryoki Mwita na kuongeza kuwa mgonjwa anaekunywa dawa tofauti na maelekezo ya mtaalam wa afya anaweza kupoteza maisha.

Sauti ya Mwita

Hata hivyo Daktari Mwita ametoa ushauri  kwa wananchi wote kuzingatia matumizi sahihi ya dawa kulingana na maelezo ya wataalamu.

Sauti ya Mwita

Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Iringa wamekiri kutumia dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kutokana na kusahau kufuata ratiba ya dawa.

Sauti ya wananchi Iringa

MWISHO