Nuru FM

Rais Samia alia ajali Mtwara

26 July 2022, 3:52 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Marco Gaguti kufuatia vifo vya watu 10 vilivyotokana na kajali ya basi la Shule.

Awali hiyo ambaye imetokea Julai 26, asubuhi ya saa moja katika eneo la mteremko la Mjimwema, Kata ya Magengeni kuelekea Mitengo, Mikindani Mkoani Mtwara.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo Jumla ya waliopoteza maisha ni 10 ambalo kuna wanafunzi wasichana 5 na wavulana 2 na watu wazima wanaume 2 ambao ni dereva wa gari hilo na msaidizi wa gari, na majeruhi ni 19 ambao capo katika hospitali ya Rufaa ya Ligula.