Nuru FM

Polisi Iringa wamshikilia Baba aliyemlawiti mwanaye wa kumzaa.

11 April 2023, 7:41 pm

ACP Allan Bukumbi akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake. Picha na Adelphina Kutika.

Mkazi wa Nzihi anakamatwa na polisi kwa kosa la kumlawiti mtoto wake wa kumzaa.

Na Adelphina Kutika

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Aman Martin Mkazi wa Kata ya Nzihi Halmashauri ya wilaya ya iringa kwa tuhuma za kumlawili mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa mwaka mmoja na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumshika mtoto kwa nguvu na kumfanyia kitendo hicho wakati wakiwa shambani baada ya mama wa mtoto kuondoka kwenda kuokota kuni na kumuacha mtoto akiwa na baba yake.

Magreth kaguo ni mama mzazi wa mtoto amekili kufanyiwa ulawiti mwanae mwenye umri wa mwaka mmoja mara baada ya kwenda kuokota kuni mlimani.

“Baba alitangulia shambani kwajili ya kuendelea na kilimo ,mimi nifuatia nyumanilivyofika shambani nikamwambia mme wanguu, nataka nikaokote kuni hapo mlimani,mme wangu akasema nenda tuu haina shida mke wangu ,nikaondoka kuokota kuni’’Alisema mama

“Nilivyorudi nilikuta mazingira ya mtoto kulia alafu nzi wamemtanda mtoto ,nikamuuliza mme wangu mbona kama sikuelewi mme wangu akajibu tupo salama

“Mtoto alisema anataka kupuu ndipo nilipogundua kuwa mtoto kalawitiwa kwa kuwa alikuwa akilia wakati wakujisaidia “Alisema mama

Mmoja wa watoto wa mama huyo ambaye ni mhanga na shuhuda wa tukio hilo la kulawitiwa kwa mdogo wake ameeleza kuwa baba yao amekuwa akiwafanyia vitendo hivyo mara kwa mara lakini mama yake hakuchukua hatua yoyote.

“kuna siku nikuwa nacheza na watoto wezangu nikawa nahitaji kunywa maji nikaingia ndani nikamkuta baba akaniambia njoo chumbani baada ya kuingia chumbani alinivua nguo na yeye akavua nguo na kutoa dudu yake na kuniingiza sehemu ya haja kubwa …mama alivyorudi nilimwambia akajibu pole.’’Alisema mtoto

MWISHO