Nuru FM

Wafungwa gereza la Kihesa Mgagao wapewa msaada

15 January 2024, 12:26 pm

Mbunge Ritta Kabati akikabidhi Msaada kwa wafungwa wa Gereza la Kihesa Mgagao. Picha na Hafidh Ally

Na Hafidh Ally

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati ametoa msaaada kwa wafungwa wa gereza la Kihesa Mgagao wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Akizungumzia kuhusu msaada alioutoa Dkt Kabati amesema kuwa Ametoa sabuni, dawa za meno, Mafuta na mahitaji mengine muhimu huku akitoa jezi na mpira Mmoja kwa watumishi wa gereza hilo.

Aidha Mh Kabati alipata Fursa ya kusikiliza changamoto za wafungwa hao huku akiahidi kutekeleza changamoto hizo kwani hata wao Wana haki ya kupata mahitaji muhimu na kutatuliwa changamoto zao.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo ameahidi kutoa shilingi Laki 5 kwa ajili ya kununua kinanda pamoja na mifuko 20 ya saruji katika kabisa la katoliki ifagi huku akiahidi kutoa mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa choo katika kabisa la Ifagi Mifugo.

“Pia nawaahidi waumini wa kanisa la KKKT usharifa wa Kihesa Mgagao nitatoa kiasi Cha shilingi Laki 5 kwa ajili ya kununulia bati” Alisema Kabati.