Nuru FM

Serikali yasikitika TRAMPA na TAPSEA kutoshiriki kikao kazi

10 May 2024, 12:32 pm

Waziri Simbachawene akiwa kwenye Zoezi la kufunga mafunzo ya uadilifu na utunzaji siri. Picha Adelphina Kutika.

Waajiri wanaoshindwa kuwapa Fursa ya kupata mafunzo waajiriwa wao waonywa ili kuongeza uelewa kwa watendaji hao.

Na Adelphina Kutika

Serikali imechukizwa na kitendo cha baadhi ya Waajiri wa Taasisi za Umma kwa kutowaruhusu na kuwagharamia Wanachama wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Wanachama wa Chama Cha Makatibu Muhsusi (TAPSEA) kushiriki kikao kazi.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, wakati akifunga mafunzo ya uadilifu na utunzaji siri kwa watunza kumbukumbu na nyaraka na makatibu mahsusi kutoka Tanzania bara na Zanzibar kwenye mkutano uliofanyika Mkoani Iringa na kusema kuwa waajiri waliokiuka maagizo ya Rais hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Sauti ya Waziri Simbachawene

Akiwasilisha taarifa mbele ya Waziri Simbachawene, Mwenyekiti wa TRAMPA, Devotha Mrope  amesema wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya waajiri kutokupokea vyema mafunzo hayo na kuwazuia  wataalamu kutoshiriki kikao kazi hicho.

Sauti ya Mrope

Gwamaka Endrew Ngomale Makamu Mwenyekiti TRAMPA Taifa amesema mafunzo hayo yamekuwa chachu kwa watunza kumbukumbu, kwani yatasaidia  kutunza siri za serikali.

Sauti ya Gwamaka

Aidha Mafunzo ya Wanachama wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) na Wanachama wa Chama Cha Makatibu Muhsusi (TAPSEA) M yalianza  may 6  2024 mpaka may 9 2024 yakiwa  na washiriki wapatao 1500 kutoka Tanzania bara na visiwani Zanzibar

MWISHO