Nuru FM

Mbunge Kiswaga atimiza ahadi ya kuwapeleka Chamgogo FC bungeni

10 November 2023, 10:13 am

Mabingwa wa Kiswaga cup 2023 Timu ya Chamgogo Fc wakiwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Na Hafidh Ally

Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh Jackson Kiswaga ametimiza Ahadi ya kuwapeleka Mabingwa wa Mashindano yake ya Kiswaga cup 2023 Timu ya Chamgogo Fc kuhudhuria Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chamgogo Fc Wamepata Fursa hiyo baada ya kuwafunga Kidamali Fc Goli 2-1 katika mchezo wa Fainali uliofanyika Katika Kijiji Cha Kalenga ambapo Mh. Kiswaga aliwaahidi kuwapeleka Bunge Kwa gharama zake kuanzia usafiri, Chakula na Malazi.

Akizungumza baada ya kutekekeza Ahadi yake. Mh. Kiswaga amesema kuwa amefurahi kuwaona vijana wakihudhuria Bunge huku akiahidi kushirikiana nao katika Miradi Mingine ya Maendeleo kwenye Jimbo la Kalenga.

Amesema baada ya safari ya Dodoma wanajiandaa kukamilisha Ahadi iliyotolewa na Katibu wa Oganizesheni ya CCM Taifa Mh Issa Gavu wakati wa uzinduzi wa mashindano yake ya kuwapeleka Visiwani Zanzibar kufanya utalii wa ndani.

Naye Mratibu wa mashindano hayo Elia Kitomo ameshukuru Mbunge kwa Ahadi yake ya kuwapeleka Mabingwa Chamgogo Fc Bungeni huku wakijipanga kuratibu safari ya Zanzibar kwa ubora.

“Kila kitu kikiwa Tayari tunataarajia timu ianze safari kuelekea Zanzibar tarehe 26 mwezi huu na huko tutafanya utalii wa ndani na kujifunza mambo mengi ya kale” Alisema Kitomo

Awali Diwani wa Kata ya Kihanga Hamis Nziku ambaye aliongozana na Timu ya Chamgogo Fc amesema ni wakati wa vijana wa Kata yake kushikamana na Mbunge wao katika kupambania maendeleo kwani wamejifunza Kiongozi Bora ni yule anayefanya Mambo kwa Vitendo.

Timu ya Chamgogo Fc ikipata Fursa ya kufanya utalii wa ndani katika Jiji la Dodoma kwa Kutembelea Ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Hospital ya Benjamin Mkapa, Nyerere Square na Kutembelea mji wa Kimkakati wa Serikali (Mji wa Magufuli).