Nuru FM

Dc Moyo aonya watakaovujisha mitihani ya darasa la saba

7 September 2021, 6:16 pm

Uongozi wa Halmshauri ya wilaya ya Iringa umesema kuwa Kuelekea mitihani ya Darasa la saba  ambayo itaanza kufanyika Sept 8 mwaka huu, vyombo vya ulinzi na usalama viko makini ili kuhakikisha mitihani inafanyika kwa amani.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed moyo alipokuwa kwenye ziara ya kukagua shule ya msingi Wenda iliyopo Kata ya Mseke  iliyopewa jina la Ulipo Nipo Toa Kero Yako Tuipatie Majawabu Sema Ukweli Na Siyo Majungu na kuongeza kuwa katika mitihani hiyo watahakikisha hakuna udanyanyifu ambao utajitokeza.

Amesema kuwa maandalizi yameshafanyika na mpaka sasa hawajasikia changamoto yoyote kutoka katika kila shule ambayo ina wanafunzi wa darasa la saba.

Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kuwa hatarajii kusikia mzazi, maafisa au walimu kujihusisha na uvujishaji wa mtihani au kutoa majibu kwa wanafunzi hao.

Kwa kweli sitarajii kuona maafisa wakijihusisha kuvujisha mtihani kwani vyombo vya ulinzi viko makini na tunatarajia wanafunzi watafanya vizuri kutokana na maandalizi ambayo wamefanya”Alisema moyo.

Aidha Mh. Moyo amesema kuwa serikali itawachukulia hatua kali wazazi ambao watawatorosha wanafunzi na kusindwa kufanya mitihani kwa kutaka kuwaozesha au kuwapeleka mijini kufanya kazi.

‘Kwa kweli serikali haitawavumilia wale wazazia ambao watawafunga ndani au kuwashawishi watoto kufanya vibaya katika mitihani hiyo, kwani serikali iko makini kwani inataka watoto wapewe ustawi mwema na huo mtihani ndio utaonesha mstakabali wa maisha yao ya baadaye, Alisema Moyo

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kuwa pia wamejipanga kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu nao wanafanya mitihani bila shida ili kutimiza malengo yao.

ii

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya msingi Wenda Mwl Jane Mkwaje amesema kuwa shule yake imejiandaa vizuri na wanatarajia wanafunzi wao watafaulu vizuri kutokana na maandalizi waliyokuwa nayo.

Amesema kuwa katika shule yake kuna jumla ya wanafunzi 77 ambapo wavulana wako 32 na wavulana wako 45 na wako tayari kwa ajili ya Mtihani huo.