Nuru FM

Wananchi Iringa waaswa kuacha kilimo Cha Bangi.

29 April 2023, 12:02 pm

Mkuu wa kitengo cha upelelezi mkoa wa iringa ISSA JUMA SULEIMANI. Picha Denis Nyali

Na Joyce Buganda

Wananchi Mkoani iringa wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kutojihusisha na kilimo cha zao la bangi linaloleta madhara kwa vijana kwani ni kosa kisheria.

Akizungumza na kituo hiki  kamishina msaidizi wa polisi ambae pia ni mkuu wa kitengo cha upelelezi mkoa wa iringa ISSA JUMA SULEIMANI amesema  zao hilo lina madhara kwani hupelekea kupoteza nguvu kazi ya vijana ambao wamekuwa  wakivuta bangi.

Amesema kuwa Vijana wanapojihusisha na uvutaji Bangi hupelekea mmonyoko wa maadili kwa vijana, ukatili wa kijinsia, magonjwa ya moyo na kuharibu Mapafu huku akiwasa vijana kutojihusha nayo.

Mkuu wa kitengo cha upelelezi  mkoa wa iringa ISSA JUMA SULEIMANI

Kamishna  ISSA ameainisha njia mbalimbali katika kuhakikisha wanakomesha kilimo cha bangi ikiwa ni pamoja na kuwatumia viongozi wa dini kutoa elimu kuhusu matumizi yake.

“Jeshi la polisi limepeleka polisi nchi nzima kuhakikisha wanatoa elimu ya madhara ya kilimo cha bangi ili kuhuisha ustawi wa jamii hasa kwa vijana” Alisema Kamishna Juma

Hata hivyo kamishna ISSA ameitaja wilaya ya kilolo kuwa ndiko ambako wanalima zao hilo hivyo amewataka kuacha mara moja kabla hatua kali hazichakuliwa dhidi yao.

Mkuu wa kitengo cha upelelezi  mkoa wa iringa ISSA JUMA SULEIMANI

MWISHO