Nuru FM

TCCIA yaiomba TRA kuwapunguzia wafanyabiashara kodi

23 May 2024, 12:27 pm

Uongozi wa TCCIA Taifa wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ofisini kwake. Picha Joyce Buganda

Licha ya wafanyabiashara kufanya kazi zao kwa mazignira rafiki Bado kumekuwa na changamoto ya kukadiriwa Kodi kubwa.

Na Joyce Buganda

Wafanyabiashara mkoani Iringa  wameilalamikia mamlaka ya mapato Tanzania  TRA kuwatoza  kodi kubwa hasa wanaposafirisha bidhaa zao kutoka mikoa ya jirani.

Wakizungumza wakati wa ziara ya Rais wa chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima TCCIA wafanyabiashara  hao wamesema wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo hiyo ya TRA wanasema VAT imekuwa ikiwatesa  jambo ambalo limekuwa likiwashusha kibiashara.

Sauti ya Rais TCCIA

Naye Rais wa Chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima TCCIA  Vicent Minja  amesema wanaangalia maendeleo ya chemba kuanzia wilayani mpaka ngazi ya mkoa , kuangalia fursa zilizopo katika mikoa lakini pia kukusanya changamoto zilizopo na kuzifanyia kazi.

Sauti ya Minja

Awali Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa iringa Edmund Mkwawa  amesema wana mpango wa kukaa kikao na wafanyabiashara kuanzia wilayani mpaka ngazi ya mkoa ili kuendelea kuiinua taasisi hiyo.

Sauti ya Mkwawa

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba  amesema kuwa serikali ya mkoa itakuwa tayari  kushirikiana na chemba hiyo ya wafanyabiashara kuleta mafanikio makubwa kwa kundi hilo.

Sauti ya Serukamba

MWISHO