Nuru FM

Madaktari bingwa kubadilishana uzoefu na watalaamu wa tiba asili

6 May 2024, 9:22 pm

Waziri wa afya Ummy mwalimu akizungumza katika Kambi ya madaktari bingwa Mkoani Iringa. Picha na Joyce Buganda.

Wataalamu hao watafanya Kazi Kaa karibu kwa ushirikiano kutoka Kwa madaktari wenyeji ili kutoa huduma za kitabibu kwa wananchi.

Na Joyce Buganda

Waziri wa afya Ummy Mwalimu amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi pindi wasikiapo uwepo wa madaktari bingwa ili kupata matibabu na kuwapunguzia gharama kubwa za kufuata wataalam mbali na maeneo yao.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango kabambe wa Madaktari Bingwa wa Dk Samia kila halmashauri hapa nchini katika Hospitali ya wilaya ya Frelimo wakiweka kambi ya siku 5 Waziri Ummy Mwalimu amesema serikali imedhamiria kupeleka madaktari bingwa katika halmashuri hizo lengo ni kuhudumia wananchi pamoja na kubadilishana uwezo na madaktari wenyeji.

Aidha Waziri Ummy amebainisha kuwa Rais Dk Samia ameandika rekodi dunia ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kwa asilimia 80 changamoto iliyosalia ni kupunguza vifo vya watoto wachanga  hivyo mpango huu wa madaktari bingwa wa dr samia utaleta suluhu kwa kuanzishwa wodi mahususi ili kuokoa maisha ya watoto wachanga.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Heri James Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema zaidi ya bilioni 27 zinatarajiwa kuletwa na serikali ili kusaidia vifaa tiba, dawa na miradi ya afya katika kuhakikisha sekta ya afya inafanya vizuri katika Mkoa wa Iringa.

Kiongozi wa kambi ya Madaktari Bingwa wa Dr Samia akizungumza kwa niaba ya madaktari wenzie amesema jopo hilo lipo tayari kutoa huduma maeneo yote na kuomba ushirikiano kutoka kwa wananchi na viongozi ili kufanikisha dhamira ya serikali.

Kambi hiyo ya Madaktari ya siku 5 imezinduliwa kitaifa Mkoa wa Iringa na inaendelea kwa nchi nzima kwa hospitali za wilaya 184 huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo TUMEKUFIKIA KARIBU TUKUHUDUMIE.

MWISHO