Nuru FM

Maagizo ya Nape Taasisi za Serikali

26 July 2022, 3:48 pm

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameagiza, taasisi za serikali kushikamana, ili kwenda pamoja kuhakikisha sekta ya habari inakua kiuchumi.

Waziri Nape ametoa rai hiyo wakati akizungumza kwa njia ya mtandao katika kikao kazi cha wakuu wa taasisi na watendaji wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Ameagiza wakuu wa taasisi wasikubali kumuona mtu akishuka, badala yake wawe na upendo na washikane mkono kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo na kuzitatua.

Waziri Nape amesema ikiwa taasisi za serikali zitashikamana, zitaweza kukua zaidi, ikiwemo kuwezesha Wizara ya Habari kujulikana kwa kazi zinazofanywa, badala ya kusubiri mojawapo kuanguka.

Aidha amewataka wakuu wa taasisi, kubuni mbinu mpya za utatuzi wa changamoto za watumishi ikiwemo kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta za habari.