Bonanza la Mahuninga latatua changamoto za wananchi
19 May 2026, 19:21

Na Joyce Buganda
Diwani wa Kata ya Mahuninga wilaya ya iringa Michael Vahaye ameandaa hafla kwa watumishi wa kata hiyo kwa kuandaa bonanza lilohusisha watumishi wa kata ya mahuninga Wilaya ya Iringa na wanafunzi yenye lengo la kutatua changamoto zilizopo kwenye kata hiyo.
Akizungumza wakati wa bonanza Hilo Diwani wa Kata ya Mahuninga Mh. Michael Vahaye amesema kwenye kata yake Kuna changamoto nyingi hivyo alimtafuta mdau ambae amemsaidia kiasi cha milion 2 na elfu 53 ambayo itasaidia kutatua changamoto mbalimbali kwenye kata hiyo.

Kwa upande wake Mdau wa maendeleo Bw. Fadhil Mgeni amesema yeye kama mpenda maendeleo ameamua kusaidia jamii iliomzunguka hivyo kidogo alichonacho.
Pia Bw. Mgeni amewaomba wadau wengine kuwa na utaratibu wa kurudi kwenye jamii zao na kutoa Chochote walichojaaliwa Ili waendelee kupata baraka zaidi.
Katika bonanza Hilo michezo mingi ilichezwa ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba na mpira wa miguu baina ya timu ya watumishi wa kata ya mahuninga na wanafunzi mechi iliyomalizka kwa kufungana magori 2 _1 huku watumishi wakiibuka na ushindi.