Nuru FM

Mikopo ya IDYDC yafungua Fursa za ajira Iringa

29 May 2026, 09:23

Mzee Brown Lalika Mkazi wa Mwang’ingo ambaye ni mnufaika wa Mikopo Kutoka IDYDC. Picha Na Hafidh Ally

Wananchi mkoani Iringa wameendelea kunufaika na mikopo inayotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la IDYDC, hali iliyosaidia kuinua uchumi wa familia nyingi kupitia uanzishaji na upanuzi wa biashara mbalimbali.

Na Hafidh Ally

Hatua ya Shirika lisilo la Kiserikali la IDYDC kutoa mikopo kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa imeendelea kuleta matumaini mapya kwa familia nyingi.Mwanahabari wetu Hafidh Ally ametuandalia makala fupi kuhusu wanufaika wa Mikipo hiyo wakizungumza hali walizokuwa nazo baada ya kupata mikopo hiyo.

Bi. Immelda Mnyawani Mkazi wa Kigonzile ambaye ni Mnufaika wa Mikopo kutoka IDYDC akiwa katika biashara yake.