Nuru FM

Mzize kufanya bonanza la washike Mkono Iringa

15 June 2026, 19:38

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James akiwapokea Clement Mzize na Oscar Evalisto katika Ofisi zake Mjini Iringa. Picha na Hafidh Ally

Bonanza hilo linatarajiwa kufanyika Tarehe 12.07.2026 Mkoani Iringa kwenye uwanja wa Samora

Na Hafidh Ally

Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, ametangaza kufanya bonanza mkoani Iringa mara baada ya ligi kuisha kwa lengo la kurudisha shukrani kwa jamii na kuwafariji watu wenye mahitaji.

Tamasha hilo litafanyika tarehe 12/7/2026 limelopewa jina la “Washike Mkono” linahusisha shughuli za kijamii ikiwemo kutembelea hospitali na kutoa msaada wa vifaa vya matibabu ikiwemo Mashine ya Utra sound, sambamba na kutembelea shule kwa ajili ya kuboresha vyoo.

Akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James, Mzize ambaye aliongozana na mshambuliaji Oscar Evalisto amesema kuwa licha ya kufikisha Vifaa hivyo kwa shule na hospital, pia atakutana na madereva bodaboda ambao aliwahi kufanya nao kazi kabla ya kugeukia soka na kuwakabidhi helment kwa usalama wao pindi wakitekeleza majukumu yao.

Sauti ya Mzize

Aidha Mzize amewataka wazazi kutowakata za watoto wao kucheza mpira kwani kwa sasa vipaji ndio sababu ya kukuza uchumi wa vijana.

“Mimi ninawasihi wazazi wasijekuruhusu vipaji vya vijana  vipotee na badala yake wawaruhusu kucheza mpira” Alisema Mzize

Aidha Mzize amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Bonanza la Tuwashike Mkono lililoandaliwa na Taasisi ya Mzize Foundation ambalo Linatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa Julai 12 2026 katika uwanja wa Samora.

Mzize amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na wachezaji mahiri wanaocheza ligi kuu Tanzania bara huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika bonanza hilo kupata burudani ya mchezo wa mpira wa miguu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amempongeza Mzize kwa kurejea Mkoani Iringa kurejesha kwa jamii huku akiridhia kuwa mgeni Rasmi katika Bonaza hilo huku akiwataka vijana wa Mkoa wa Iringa kuiga mfano wa Mzize ambaye ameonesha nidhamu katika mchezo wa soka.

Amesema kuwa Mzize Ameutangaza mkoa wa Iringa kupitia mchezo wa soka, ambapo amesema kuwa Serikali ya Mkoa wa Iringa imejipanga kishirikiana na mchezaji huyo kufanikisha Bonanza lake.

Sauti ya RC Kheri James

Awali Mkurugenzi wa Young stars Sports Academy Mkoani Iringa Said Chitalula ambaye pia ni Mlezi wa Mchezaji Clement Mzize amesema kuwa kupitia Bonanza hilo wazazi na wakazi wa Iringa wataweza kuelewa kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ajira kwani kwa sasa wanajivunia Mchezaji huyo ambaye anaendesha maisha yake kupitia mpira wa Miguu.

Sauti ya Chitalula
Wachezaji Clement Mzize na Oscar Evalisto wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa