Nuru FM

SHIVYAWATA Iringa kuandaa kongamano la wenye ulemavu

1 October 2026, 14:19

Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Mkoa wa Iringa, Shabani Shomari akizungumzia Kongamano la wenye ulemavu. Picha na Hafidh Ally

Kongamano hilo linatajwa kuwawonesha watu wenye ulemavu fursa za kujikwamua kiuchumi.

Na Hafidh Ally

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania, SHIVYAWATA, Mkoa wa Iringa, inaandaa kongamano pamoja na maonesho ya bidhaa na huduma zinazotolewa na watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu mwaka 2026.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba katika Viwanja vya Garden, Manispaa ya Iringa, likiwa na lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki, uwezo, fursa na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Mkoa wa Iringa, Shabani Shomari, amesema kongamano hilo litatoa fursa kwa watu wenye ulemavu kuonesha bidhaa, huduma, vipaji na ubunifu wao, hatua itakayowasaidia kujitangaza na kupanua fursa za kiuchumi.

Sauti ya Shabani Shomari

Amesema SHIVYAWATA inawakaribisha wadau mbalimbali kushiriki na kuunga mkono kongamano hilo ili kuhakikisha linafikia malengo yaliyokusudiwa.

Sauti ya Shabani Shimari

Aidha, amewataka watu wenye ulemavu kutumia fursa hiyo kuonesha uwezo wao na bidhaa wanazozalisha, huku jamii ikihimizwa kutambua na kuthamini mchango wao katika maendeleo.