Nuru FM

Watu 21 wafariki dunia, watano wajeruhiwa katika ajali Iringa

9 November 2026, 14:42

Basi la Abiria la Kampuni ya Maokoto lililopata ajali leo. Picha na Hafidh Ally

Waliofariki dunia ni wanaume 10, wanawake tisa na watoto wawili, huku watu wengine watano wakijeruhiwa katika ajali hiyo.

Na Hafidh Ally

Watu 21 wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria na lori, iliyotokea eneo la Njiapanda ya Kiponzero, kwenye Barabara Kuu ya Iringa–Mbeya mkoani Iringa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, ajali hiyo imetokea baada ya basi la abiria la Kampuni ya Maokoto lililokuwa likitoka Kijiji cha Wasa, Wilaya ya Iringa, kuelekea Iringa Mjini, kudaiwa kupata hitilafu katika mfumo wa breki wakati likitokea barabara ya vumbi na kuingia Barabara Kuu, hali iliyosababisha dereva kushindwa kulidhibiti na kugongana na lori.

Sauti ya Kamanda Bukumbi

Kamanda Bukumbi amesema majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na Hospitali ya Ipamba.

Sauti ya Kamanda Bukumbi

Aidha, Kamanda Bukumbi amewataka madereva kuzingatia sheria na kuchukua tahadhari wanapotumia barabara, hususan katika maeneo ya makutano ya barabara, ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha vifo na majeraha.

Sauti ya Kamanda Bukumbi