Nuru FM

Serikali yahimiza wanawake vijijini kupata fursa sawa za umiliki mali

15 October 2026, 10:31

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake, Regina Molleli akizungumzia fursa za umiliki mali kwa wanawake. Picha na Chacha Robert

Wanawake wanapopewa fursa za kumiliki rasilimali za uzalishaji wana uwezo wa kuchangia kikamilifu maendeleo ya jamii na taifa.

Na Chacha Robert

Serikali imetoa wito kwa jamii na wadau wa maendeleo kuhakikisha wanawake wa vijijini wanapewa fursa sawa za kumiliki na kupata rasilimali za uzalishaji mali, zikiwemo ardhi, mitaji na teknolojia za kisasa za kilimo, ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kufanikisha Dira ya Taifa ya 2050.

Akizungumza katika Kijiji cha Vitono, Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mwanamke Anayeishi Kijijini, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake, Regina Molleli, amesema maadhimisho hayo yanalenga kutambua mchango wa wanawake wa vijijini katika uzalishaji mali, maendeleo ya familia na ukuaji wa uchumi wa taifa.

Sauti ya Mollel

Kwa upande wake, Wakili Isabella Nchimbi kutoka Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), amesema licha ya sheria kutambua haki za wanawake katika umiliki wa mali na ushiriki katika maamuzi, baadhi ya mila na desturi bado zinawanyima wanawake fursa hizo, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki zao.

Sauti ya Wakili Isabella

Naye Mratibu wa Maadhimisho hayo kitaifa na Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka wizara hiyo, Josiah Saoke, amesema serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu haki za wanawake na sheria zinazowalinda, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza ukatili wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kupata haki zao.

Sauti ya Saoke Mratibu wa maadhimisho

Mshiriki wa maadhimisho hayo kutoka Kata ya Uhambingeto, Kijiji cha Kipaduka, Esther Menadi, amesema wanawake wa vijijini bado wanakabiliwa na changamoto za kumiliki ardhi, akiiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wanawake wapate fursa ya kumiliki ardhi na kujitegemea kiuchumi.

Sauti ya Manedi Mshiriki