Wakazi wa Mtaa wa uwanja wapondwa mawe na watu wasioonekana
15 December 2022, 8:15 pm
Na Mrisho Sadick
Wakazi wa Mtaa wa Uwanja Kata ya Nyankumbu wilayani na Mkoani Geita wamekumbwa na taharuki kufuatia tukio la kurushiwa mawe ya ajabu kwenye makazi yao na watu ambao hawaonekani nyakati za mchana na usiku hali ambayo imeendelea kuwapa wasiwasi nakuiomba serikali ya mtaa kuingilia kati kuwasaidia.
Inaelezwa kwamba tukio hilo limedumu kwa muda wa siku saba, nakwamba licha yakutokuwepo kwa madhara ya kibinadamu kuna uharibifu wa nyumba ikiwemo kuvunjwa kwa vioo vya madirisha pamoja na mabati kutobolewa.
Storm FM imefika eneo la tukio nakufanikiwa kuzungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo juu ya tukio hilo la kushangaza ambalo linahusishwa na imani za kishirikina ambapo mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa uwanja Enos Chelehani amefika eneo la tukio nakukiri kuwepo kwa tukio hilo.
Diwani wa kata ya Nyankumbu lilipotokea tukio hilo Jonh Mapesa amefika eneo la tukio nakuwataka wakazi wa eneo hilo kuwa wavumilivu wakati serikali inalifanyia kazi suala hilo.
.