Storm FM

Wimbi la wizi lawaibua wananchi Nyamakale

19 November 2024, 10:53 am

Baadhi ya wananchi wakiwa ofisi ya polisi jamii wakitambua vitu vyao vilivyoibiwa. Picha na Kale Chongela

Vilio vya wananchi kwa serikali juu ya kuongezeka kwa wimbi la vijana wezi katika mtaa wa Ibolelo Mwabasabi Kata ya Nyankumbu mjini Geita.

Na Kale Chongela:

Wakazi wa Nyamakale Mtaa wa Ibolelo maarufu kwa jina la Mwabasabi  Kata ya Nyankumbu Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita wamedai kukithiri kwa wimbi la wizi linalofanywa na watu wasiojulikana hali ambayo inawatia wasiwasi.

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo novemba 08,2024 wameiambia Storm FM kuwa vitendo hivyo vimeedelea kushika kasi huku wakiiomba serikali kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa huo kuchukua hatua za haraka kukomesha vitendo hivyo kwani vinawarudisha nyuma kimaendeleo.

Sauti ya wakazi wa Ibolelo
Badhi ya vitu vilivyodaiwa kuibiwa sehemu mbalimbali za mtaa wa Ibolelo na watu wasiyojulikana vikiwa ofisi ya polisi jamii. Picha na Kale Chongela

Balozi wa shina namba 9  Bw Baraka Masami  amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo nakwamba katika tukio la kukamatwa kwa baadhi ya vitu mbalimbali vilivyoibiwa amewapongeza wananchi na polisi jamii kwa kuendelea kupambana vikali dhidi ya vitendo hivyo huku akiahidi kulifikisha suala hilo kwa viongozi wa ngazi za juu kwa ajili ya utatuzi zaidi.

Sauti ya Balozi

Katibu wa polisi Jamii mtaa wa mwabasabi Bw Deusi Paulo Masusu  amebainisha kuwa baada ya kubaini kuwa  kuna mali za wizi zimekamata alianza kutoa taarifa katika mitaa jirani ili kupata wahusika wa mali hizo zilizokamatwa huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa za viashiria vya vitendo vya uhalifu ili waone namna ya kuvidhibiti kwa kushirikiana na Jeshi la polisi.

Sauti ya katibu polisi Jamii