Storm FM

Mwenge waweka jiwe la msingi barabara yenye KM 1.24 Bukombe

2 October 2024, 10:24 am

Jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za UyovuHC, Runzewe SEC na Matenkini. Picha na Kale Chongela.

Mwenge wa uhuru unaendelea kutembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Geita tangu ulipopokelewa Septemba 30, 2024.

Na: Kale Chongela – Geita

Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika barabara inayojegwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 1.24 kutoka Uyovu hadi shule ya sekondari Runzewe wilayani Bukombe mkoani Geita.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo  Okitoba mosi, 2024 meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) wilaya ya Bukombe mhandisi Msoka Msumba amesema, Mradi huo una thamAni ya shilingi  891,607, 500 na kwamba  unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.

Sauti ya meneja TARURA

Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe. Paskasi Muragili amesema mradi huo utakuwa chachu kuwarahisishia watumiaji wa barabara hiyo ikiwemo watumiani wa vyombo vya moto.

Sauti ya DC Bukombe

Akiwa katika mradi huo mara baada ya kufanya ukaguzi kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mzava ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi  katika  mradi huo huku akiwasihi kuongeza jitihada zaidi ili mradi huo ukamilike kwa muda uliopangwa.

Sauti ya Godfrey Mzava