Shule za Msingi Geita zatakiwa kufanya mijadala
25 April 2021, 2:27 pm
Walimu shule za msingi katika halmashauri ya mji wa Geita wameshauriwa kuandaa mijadala shuleni baina ya shule jirani ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa kujieleza kitaaluma .
Ushauri huo umetolewa na Afisa tawala Wilaya ya Geita Bw Inocent Mabiki ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mjadala uliofanyika katika kata ya Nyankumbu na kuzikutanisha shule 6 kwa lengo la kushindana kwa hoja na kupanuaulewa kwa wanafunzi.
Mdahalo huo ulikuwa unahusu uzalendo kwa watanzania na shule ya msingi Mbugani imeibuka mshindi kwa 90% dhidi ya shule ya msingi Nyankumbu iliyopata 80% na wanafunzi wa shule zote shiriki kusema kuwa k suala hili likizingatiwa na kutiliwa mkazo litawasaidia wanafunzi kuendelea kufanya vizuri.
Kwa upande wake afisa utamaduni halmashauri ya mjii wa Geita Bi Ngianasia Kisamo amesema watahakikisha wanasimamaia zoezi hilo liwe endelevu katika halmashauri zote ili na kufanyika kwa mujibu wa taratibu za TAMISEMI.