Wananchi wakwama kisiwani kisa kivuko
13 March 2024, 4:20 pm
Ukosefu wa kivuko cha uhakika katika visiwa mbalimbali hapa nchini imekuwa changamoto kwa wnanchi kufanya shughuli za uchumi
Wakazi wa kisiwa Cha Izumacheli wilayani Geita wamedai kukabiliwa na Changamoto ya usafiri wa Kutoka katika kisiwa hicho baada ya ferry waliyokuwa wakiitumia kupunguziwa ruti ya kwenda katika eneo hilo.
Kisiwa hiki Cha Izumavcheli mbali nakuwa na visiwa vingine vidogo vidogo ndio makao makuu ya Kata ya Izumacheli yenye wakazi zaidi ya watu 6,000 wameiangukia serikali kuongeza ruti za ferry ya MV TEGEMEO kwani tangu zipunguzwe kutoka ruti mbili hadi moja kwa siku wamekuwa wakipata changamoto.
Diwani wa Kata hiyo Cosmas Fideli amesema baadhi ya wakazi wa kisiwa hicho hawatoki kwenye kisiwa huku Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Msukuma akieleza changamoto iliyowakumba wakati wakitumia Boti kufika katika Kisiwa hicho.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Tanzania Fadhili Maganya kufika katika eneo hilo Kuangazia changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi hao ikiwa ni Kiongozi wa kwanza wa Kitaifa kufika Kisiwani humo huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Nicholous Kasendamila akimuagiza Mbunge msukuma kufuatilia nakuchukua hatua za changamoto ya kivuko hicho.