Mazingira FM
Mazingira FM
21 February 2026, 12:17 pm

Wanafunzi wametakiwa kujitahidi katika masomo yao ili kuandaa taifa na viongozi bora wa baadaye.
Na Taro Michael Mujora
Wanafunzi wametakiwa kujitahidi katika masomo yao ili kuandaa taifa na viongozi bora wa baadaye.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Sulum Alfan Mtelela katika mdahalo wa wazi uliofanyika katika Shule ya sekondari Bunda, kwa kusema juhudi za kisomo ni nguzo muhimu ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha mtaaluma wa shule ya sekondari Bunda Baraka Charles Wambura amewaomba wazazi na walezi kushirikiana kwa karibu na walimu, ili kupunguza changamoto zinazowasababisha baadhi ya wanafunzi kuacha shule kwa kusistiza mshikamano huo ni muhimu ili kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora na mazingira salama.

Kwa upande wao, wanafunzi Noela Paschal Lucas na Erick Boniphace Andrea walisema wamejifunza mengi kupitia mdahalo huo. Walisema kwamba mwanafunzi anayekatiza masomo yake anakabiliwa na hatari ya kutopata ajira na kuongezeka kwa migogoro katika familia Pamoja na kusisitiza kuwa ushirikiano mkubwa kati ya wazazi, walimu na wanafunzi ni muhimu.