Mazingira FM
Mazingira FM
10 April 2026, 14:00

Mambo ya kuzingatia wakati wa kuandaa habari, vyanzo vya habari na mambo ya kuzingati wakati wa kuhariri habari.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetoleawa kwa jamii kufuatalia vyombo vya habari kutokana na umuhimu wake kwa jamii hasa katika kupasha habari za uhakika na ukweli
Wito huo umetolewa na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Migungani iliyopo kata ya Bunda stoo wilaya ya Bunda mkoani Mara katika ziara yao studio za radio mazingira fm

Ziara ya wanafunzi hao ililenga kujifunza namna vyombo vya habari vinafanya kazi zao katika kupeleka elimu kwa jamii na umuhimu wa vyombo vya habari hasa radio katika jamii.
miongoni mwao wameeleza kujifunza mambo kadhaa ikiwepo mambo ya kuzingatia wakati wa kuandaa habari, vyanzo vya habari na mambo ya kuzingati wakati wa kuhariri habari.