Mazingira FM
Mazingira FM
2 April 2026, 17:51

ASP Buhembere: “Chanzo kikuu cha ajali ni matendo ya kibinadamu, mazingira na chombo chenyewe hivyo.”
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wamiliki wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanakuwa na bima za vyombo hivyo ili kukidhi matakwa ya kisheria kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 168 cha sheria ya usalama barabarani na kifungu cha 169 cha sheria ya bima.
Hayo yamebainishwa leo na Mrakibu msaidizi wa polisi ASP Faustin J. Buhembere na mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Bunda kupitia kipindi cha asubuhi leo mazingira fm ambapo amesema chombo cha moto chenye bima hata kikipata ajali waathirika wanapata fidia kupitia bima hiyo.
ASP Buhembere ameongeza kuwa madereva kwa kiasi kikubwa ndiyo wanaowajibu kuhakiki chombo cha moto kabla ya kukitumia wanajiridhisha kuwa kina bima lakini na dereva mwenyewe awe na leseni.
ASP Buhembere amesema chanzo kikuu cha ajali ni matendo ya kibinadamu, mazingira na chombo chenyewe hivyo Pamoja na kuwa wanaweka na kusimamia sheria za usalama barabarani bado kuna watu wanavunja sheria hizo.

Kwa upande wake Halfan Isango Afisa ubora kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania TIRA kanda ya ziwa amesema wao kama TIRA wanasimamia wa bima wanasimamia masuala mbalimbali ikiwemo kutoa ithibati kwa mawakala wa utoaji huduma za bima ikiwemo vyombo vya moto
Isango pia amesema jukumu linguine ni kutoa elimu kwa jamii na wamiliki na watumiaji vyombo vya moto kujua umuhimu wa vyombo hivyo pia kushughulikia malalamiko yote yanayohusu bima.