Mazingira FM

Watakiwa kuwahi hospitali wanapoona dalili za nimonia

14 March 2026, 13:04

Dkt.Regnand Milinga akiwa studio za radio Mazingira FM.

Dkt.Regnand Milinga wito kwa wananchi endapo mtu ataonekana na dalili za nimonia ni muhimu kufika kituo cha kutolea huduma za afya kwani ugonjwa huo ni hatari na ni rahis kusababisha kifo

Imeelezwa kuwa kati ya magonjwa ambukizi yanayosababisha vifo hasa kwa watoto chini ya miaka mitano na watu wazima juu ya miaka 65 ni ugonjwa wa nimonia.
Hayo yameelezwa na dkt.Regnand Milinga kutoka Ukombozi dispensary akizungumza kwenye kipindi cha kapu letu mazingira fm akitoa elimu ya afya kuhusu ugonjwa wa nimonia.
Ambapo amesema ugonjwa wa nimonia unasababishwa bakteria , virusi na fangasi ambavyo vinagawanya ugonjwa huo katika makundi mbalimbali.

Sauti ya dkt.Regnand Milinga kutoka Ukombozi dispensary

Aidha ameeleza mtu anaweza kuona dalili ndani ya saa 48 ,ambapo ni kama homa kali,kikohozi na maumivu ya kifua.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi endapo mtu ataonekana na dalili za nimonia ni muhimu kufika kituo cha kutolea huduma za afya kwani ugonjwa huo ni hatari na ni rahis kusababisha kifo.

Sauti ya dkt.Regnand Milinga kutoka Ukombozi dispensary