Mazingira FM

Uchakavu wa miundombinu waitesa shule ya msingi Tingirima

26 February 2026, 10:06

Jumla ya wanafunzi 850 kutumia vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu mawili ya vyoo.

Na Mariam Mramba

Shule ya msingi Tingirima iliyopo kata ya Mugeta halmashauri ya wilaya ya Bunda inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ikiwemo vyumba vya madarasa pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo hali iliyopelekea jumla ya wanafunzi 850 kutumia vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu mawili ya vyoo.

Hayo yamebainika jana february 25 2026 wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo hilo Boniphace Mwita Getere yenye lengo kuwashukuru wananchi pamoja na kukaguwa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo alibaini kuwa wanafunzi wa shule hiyo wanapta adha kutokana na hali iliyopo shuleni hapo

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Tingirima wamemuomba mbunge wa jimbo hilo Bonophace Mwita Getere awasaidie kutatua changamoto zilizpo kijijini hapo ikiwemo ya uchakavu wa miundombinu ya shule, kuwasaidia kupatikana kwa maji shuleni pamoja na ujenzi wa zahanati ya kijiji.

Boniphace Getere amesema kuwa katika kutatua changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya shule tayari amewasilisha changamoto hiyo kwa waziri wa Tamisemi ambapo pia amewahamiza viongozi wa kijiji hicho kuharakisha ukamilishaji wa mradi wa chumba kimoja cha darasa unaotekelezwa katika shule hiyo ili jengo hilo lianze kutumika kutokana na madarasa yaliyokuwepo kutitia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Sauti ya Boniphace Mwita Getere

Aidha katika ziara hiyo katika kata ya Mugeta mbunge amekagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shule ya msingi Kyandende matundu 12 ya vyoo shule ya msingi Kyandege, zahanatati ya Kyandege ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya msingi Tingrima matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Tingirima pamoja na kusikiliza kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara.