Mazingira FM
Mazingira FM
19 February 2026, 12:49 pm

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara limepitisha bajeti yenye jumla ya shilingi bilion 38,947,705,000
Na Edward Lucas
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara limepitisha Bajeti yenye jumla ya Shilingi bilion 38,947,705,000 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Kati ya fedha hizo, Tshs 2,892,532,000 ni mapato ya ndani, Tshs 1,864,508,000 ni ruzuku na matumizi mengineyo, Tshs 26,503,644,000 ni ruzuku ya mishahara, na Tshs 7,687,021,000 ni ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu pamoja na wahisani mbalimbali.
Akisoma bajeti hiyo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Renats Mjungu Mjungu amesema Pamoja na kupitishwa kwa bajeti hiyo ya halmashauri pia baraza hilo limepitisha bujeti ya tarura ambayo ni billion 7.5 na ruwasa ikiwa ni shilingi billion 2.5.
Kwa upande wake mkuu wawila ya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge amewataka viongozi na watumishi wa halmashauri kuzingatia nidhamu naweledi katika utekelezaji wa bajeti iliyopitishwa.