Mazingira FM

NMB yakabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya mil 230 mkoa wa Mara

31 January 2026, 12:12 pm

wakati viongozi NMB wakikabidhi Encubator

Katika msaada huu Benk ya NMB imetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 230 mkoani Mara ambapo  kwa hospital DDH Rorya imepokea Encubators 8 ambazo zitasaidia watoto njiti baada ya kuzaliwa.

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa ukosefu wa  vifaa saidizi kwa watoto njiti ( Encubators) husababisha vifo kwa asilimia 40 wilayani Rorya ambapo katika hospital moja watoto 280 wanaozaliwa kwa mwezi watoto 30 kati yao huzaliwa chini ya umri.

Hayo yamesemwa na Dr Halfan Haule mkuu wa wilaya ya Rorya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara Mhe Kanal Evans Mtambi katika hafla ya kupokea vifaa vya hospitali na shule kutoka Bank ya NMB

Dkt Halfani kwa niaba ya mkuu wa mkoa ameishukuru bank hiyo kwa  msaada huo walioutoa kwa hospitali na shule ndani ya mkoa wa Mara huku akitoa wito kwa waliopokea vifaa kuhakikisha vinatumika kama malengo yaliyokusudiwa.

Sauti ya Dr Halfan Haule mkuu wa wilaya ya Rorya
wakati mkuu wa wilaya akikabidhi mashuka na magodoro kwa mkurugenzi wa manispaa ya Musoma

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi na Afisa mkuu wa fedha wa Bank ya NMB Juma Kimori amesema bank hiyo imeendelea kuiunga mkono serikali katika kusaidia sekta za elimu, afya pamoja na majanga.

Katika msaada huu Benk ya NMB imetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 230 mkoani Mara ambapo  kwa hospital DDH Rorya imepokea Encubators 8 ambazo zitasaidia watoto njiti baada ya kuzaliwa.

Kimori amesema tangu NMB ianzishwe hadi mwaka 2025 jumla ya shilingi bilion 23 zimetolewa na bank hiyo kurudisha shukrani kwa wananchi.

Sauti ya Mkurugenzi na Afisa mkuu wa fedha wa Bank ya NMB Juma Kimori
Wakati NMB wakikabidhi viti na meza kwa viongozi wa Mara

Kwa upande wake Dr Bwire Chirangi Mganga mkuu hospitali ya Menonite Shirati Rorya amesema  uwepo wa vifaa hivyo utasaidia kwa kiwango kikubwa kuhudumia akina mama wanaojifungua watoto njiti katika eneo hilo.

Aidha ameiomba serikali kuiongezea hospitali hiyo watumishi kutokana na mahitaji yaliyopo akidai zaidi ya wauguzi 10 waliyokuwa wakitoa huduma hospitalini hapo wameondoka baada ya kuajiriwa na serikali.

Sauti ya Dr Bwire Chirangi Mganga mkuu hospitali ya Menonite Shirati