Mazingira FM

CCM Balili yatoa siku saba kwa shule mbili maboresho ya vyoo

27 August 2024, 12:49 pm

Mkuu wa shule ya sekondari Rubana mwenye suti akitoa maelezo kwa viongozi wa chama, Picha na Adelinus Banenwa

Siku saba zimetolewa na katibu mwenezi CCM Balili kwa shule ya msingi na sekondari Rubana kufanya marekebisho ya vyoo vya wanafunzi ikiwa ni pamoja na huduma ya maji ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Na Adelinus Banenwa

Chama cha mapinduzi CCM kata ya Balili kupitia kwa katibu wa siasa na uenezi wa kata hiyo wametoa siku 7 kwa uongozi wa shule za msingi na sekondari Rubana kufanya marekebisho kwenye vyoo vya wanafunzi ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kutokea.

mwalimu mkuu msaidi shule ya msingi Nyerere akiwapitisha wageni kwenye maeneo ya shule kwenye ziara ya katibu mwenezi Balili, Picha na Adelinus Banenwa

Akizungumza na Mazingira fm Edward Emmanuel Nyamanyi katibu wa siasa na uenzi CCM Balili amesema amefanya ziara katika shule zinazopatikana kwenye kata yake lakini mbali na changamoto zingine wamebaini hali ya vyoo haikuwa nzuri hasa shule za Rubana sekondari na Rubana shule ya msingi.

Sauti yaEdward Emmanuel Nyamanyi katibu wa siasa na uenzi CCM Balili
Hali ya vyoo shule ya sekondari Rubana kukosa maji, , Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Nyamanyi amesema ziara hizo zitakuwa za mwendelezo katika kuhakikisha serikali inayosimamiwa na chama cha mapinduzi inafanya kazi kama ilani ya uchaguzi inavyoelekeza katika kata hiyo.