Mazingira FM

Kundo amtaka mkadarasi wa mradi wa maji taka Bunda kuukamilisha kwa wakati

24 July 2024, 7:02 am

Naibu waziri wa Maji Mhe Kundo Andrew Mathew, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa mradi wa maji taka Bunda, Picha na Adelinus Banenwa.

Naibu waziri wa Maji Mhe Kundo Andrew Mathew amemtaka mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa maji taka kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Na Adelinus Banenwa

Naibu waziri wa Maji Mhe Kundo Andrew Mathew amemtaka mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi wa maji taka kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Mhe naibu waziri amesema hayo leo July 23, 2024 katika ziara yake mjini Bunda ambapo ametembelea mradi huo wa maji taka unaojengwa katika kata ya Bunda stoo mtaa wa Butakale mjini Bunda unaogharimu shilingi bilioni 1.7.

Aidha mhe naibu waziri amesema uwepo wa eneo la kukusanya maji taka utawezesha mji wa Bunda kuwa msafi na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

sauti ya Naibu waziri wa Maji Mhe Kundo Andrew Mathew

Ujenzi wa mradi wa maji taka butakale unajengwa na mkandarasi Patrick kashere na mradi huo unatarajia kukamilika mwezi November mwaka huu.