Mazingira FM

Mabotto atoa mkono wa pasaka kwa wagonjwa Manyamanyama

1 April 2026, 19:13

Umekuwa ni utamaduni wa kiongozi huyo kwa zaidi ya miaka nane sasa amekuwa akitoa misaada kwa makundi mablimbali hasa kuelekea siku za sikukuu”.

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa zamani wa jimbo la Bunda mjini na mkurugenzi wa Mabotto Microfinence ndugu Robert Chacha Maboto ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa na akinamama waliojifungua hospitali ya Manyamanyama

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi huyo, Emmanuel Kija amesema umekuwa ni utamaduni wa kiongozi huyo kwa zaidi ya miaka nane sasa amekuwa akitoa misaada kwa makundi mablimbali hasa kuelekea siku za sikukuu ikiwa ni pamoja na mahospitalini na vituo vya afya, magereza nk

Aidha Emamanuel amewapongeza madaktari Pamoja na wauguzi wa hospitali ya Manyamanyama ambao wameendelea kufanya kazi yao bila kuchoka licha ya kuwa na changamoto mabalimbali.

Sauti ya Emmanuel Kija

Kwa upande wao baadhi ya akina mama waliojifungua hospitalini hapo wameshukuru kwa msaada walioupata kutoka kwa mkurugenzi Maboto huku wakisifu huduna nzuri wanayopatiwa na madaktari.

Sauti za baadhi ya akina mama waliojifungua
Baadhi ya zawadi alizozitoa mkurugenzi wa Mabotto Microfinance

Naye mganga mfawidhi wa hospotali ya Manyamanyama Ndongo Vicent amesema leo hospitali hiyo imepokea msaada kutoka Mabotto microfinance ambapo ni sabuni za unga na mche, maji ya kunywa, mafuta ya kupaka, pampasi za watoto huku akibainisha kuwa vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa,

Ameongeza kuwa hospitali hiyo ya Manyamanyama kwa mwezi mmoja zaidi ya akinamama 200 hujifungua ambapo ni wastani wa akinamama 10 kila siku.

Sauti ya mganga mfawidhi wa hospotali ya Manyamanyama Ndongo Vicent