Mazingira FM
Mazingira FM
31 March 2026, 15:24

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamiii halmashauri ya Bunda Bi Octavina Kiwone ameeleza kuhusu fursa ya mikopo ya asilimia 10 ambapo amewataka vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kuunda vikundi imara vitakavyowasaidia kupata fursa hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuinua kipato chao.
Akielezea umuhimu wa waombaji mikopo kuwa katika vikundi Bi Octavina amebainisha kuwa mfumo huo huongeza uwajibikaji, mshikamano na urahisi wa usimamizi wa mikopo hivyo kuongeza uwezekano wa urahisi wa urejeshaji kwa wakati.
Bi Octavina ametoa elimu kuhusu sifa za waombaji wa mikopo kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu.
Alisisitiza umuhimu wa vikundi kusajiliwa rasmi, kuwa na mpango wa biashara wenye tija, pamoja na kuzingatia nidhamu katika urejeshaji wa mikopo ili kuwezesha watu wengi zaidi kunufaika na fursa hiyo ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri