Mazingira FM
Mazingira FM
28 February 2026, 15:04

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi, aagiza watu wote waliovamia maeneo ya Chama Kikuu cha Ushirika Pamba Mara, kuondoka mara moja
Na Thomas Masalu
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi, ameagiza watu wote waliovamia maeneo ya Chama Kikuu cha Ushirika Pamba Mara, kuondoka mara moja, akisisitiza umuhimu wa kulinda mali na rasilimali za chama kwa manufaa ya wanachama wake.
Aidha, ameagiza kuimarishwa kwa mnyororo wa thamani wa mazao yanayosimamiwa na kuratibiwa na chama hicho, hatua itakayochochea ongezeko la tija na mapato kwa wakulima.
Maagizo hayo yametolewa leo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho uliofanyika ukumbi wa Mwembeni Compelex Musoma mjini, ambapo ujumbe wake uliwasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka.
Vilevile, amehimiza matumizi sahihi na matunzo bora ya vitendea kazi vya kilimo cha pamba vilivyozinduliwa, ikiwemo trekta na pikipiki, ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kuboresha huduma kwa wanachama.