Mazingira FM

ASILI B-CC wazinduliwa, kiboko ya lishe, kilimo, tabianchi Mara

10 February 2026, 5:47 pm

Baadhi ya viogozi walioshiriki katika uzinduzi wa mradi wa ASILI B-CC,picha na Catherine Msafiri

Meneja mkaazi – Vi Agroforestry Martha Olotu amesema mradi wa ASILI B –CC unalengo la kukabiliana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na lishe duni na mabadiliko ya tabia nchi.

Na Catherine Msafiri

Shirika la Vi Agroforstry kwa kushirikiana na shirika la IDS, Bufadeso na Mviwanya wamezindua mradi wa ASILI B-CC wenye lengo la kuwainua wakulima na kuchechemua maendeleo ya kilimo.

Akizindua mradi huo mgeni rasmi mhandis Mwita Okae Chacha kaimumkuu wa sehemu ya uchumi na uzalishaji kwaniaba ya katibu Tawala Mkoa wa Mara Gerlad Kusaya amesewapongeza Vi Agroforest na kutoa wito kwa viongozi na jamii kushiki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo

Sauti ya Mhandis Mwita Okae Chacha
Meneja mkaazi – Vi Agroforestry Martha Olotu akizungumzia mradi wa ASILI B-CC,picha na Catherine Msafiri

Akielezea mambo wanayotekeleza kupitia mradi wa ASILI B Meneja mkaazi – Vi Agroforestry Martha Olotu amesema mradi wa ASILI B –CC unalengo la kukabiliana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na lishe duni na mabadiliko ya tabia nchi.

Sauti ya Meneja mkaazi – Vi Agroforestry Martha Olotu
Baadhi ya wadau walioudhulia kikao cha uzinduzi wa mradi,picha na Catherine Msafiri.

Wakitoa mawasilisho ya utekelezaji wa mradi huo viongozi kutoka mashiri ya IDS,Mviwanya na Bufadeso wamebainisha lengo la mradi huo ni kuwapa ujuzi wakulima .

Akisoma wasilisho la shirika la IDS Afisa miradi David Lukumay Minyali amebainisha shughuli zitakazotekelezwa chini yao katika Kata 7 ndani ya wilaya 2 ya Butiama na Tarime.

Kwa upande wake mratibu wa shirika la Mviwanya Joel Nguvava amesema watatekeleza katika kata 15 wilaya ya Serengeti na kata 15 katika wilaya ya Tarime ambapo mradi huo utatekelezwa kwa gharama ya Million 484

Naye mkurugenzi wa shirika la Bufadeso Baraka James Kamese amesema mradi una lengo la kuwafikia walengwa 5000 ndani ya kata 5 kwenye wilaya ya Butiama.

Sauti za viongozi wa mashirika

Hata hivyo mradi huo wa ASILI B-CC utatekelezwa ndani ya miaka 3 (2026 -2028) katika wilaya tatu za mkoa wa Mara.