Mazingira FM

Mahakama Bunda yaadhimisha siku ya sheria, sheria 446 zatafsiriwa kiswahili

3 February 2026, 6:22 am

Hakimu Mkazi Mwandamizi Mlokozi Kamuntu,picha na Catherine Msafiri

Monika hokololo Mkuu wa mashitaka wilaya ya Bunda sheria zaidi ya 400 zimetafsiriwa kwa lugha ya kiswahili kwa lengo la kuwasaidia wananchi kuelewa mambo ya kimahakama.

Na Catherine Msafiri

Imeelezwa kuwa Mahakama inaendelea na utafsiri wa sheria mbalimbali kwa lugha ya kiswahili ambapo mpaka sasa imetafsiri sheria zaidi ya 446.

Hayo yamebainishwa na Monika hokololo Mkuu wa mashitaka wilaya ya Bunda wakati akisoma lisala ya mahakama mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya sheria zilizofanyika kiwilaya katika viwanja vya mahakama ya wilaya Bunda.

Sherehe hizo zimeudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini,mawakili wastaafu na wananchi.

Monika hokololo Mkuu wa mashitaka wilaya ya Bunda,picha na Catherine Msafiri
Mkuu wa mashitaka wilaya ya Bunda

Mgeni rasmi hakimu mwandamizi Mlokozi Kamuntu akihutubia hafla hiyo amebainisha mambo yanayotekelezwa na mahakama ili kuwasaidia wananchi ikiwamo  kuanzisha njia za kutatua migogoro kama mahakama mtandao na mahakama inayotembea.

Aidha amebainisha kuwa matumizi hayo ya njia za kutatua migogoro yameleta manufaa katika mahakama

Hakimu mwandamizi mlokozi kamuntu

Mgeni wa heshima katibu tawala wa wilaya ya Bunda Salum Alfan Mtelela akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Kaminyoge ameipongeza mahakama kwa kuendeleza siku ya sheria ambapo inasaidia wananchi kupata elimu.

Ametumia jukwaa hilo kutoa wito kwa wananchi kuendeleza umoja na amani ili kuepuka yaliotokea 29 october,2025 yasitokee tena.

Katibu tawala wa wilaya ya Bunda Salum Alfan Mtelela

Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitaifa yamefanyika katika makao makuu ya Mahakama ya Tanzania mkoani Dodoma.mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi.