Mazingira FM

TMO Bunda: “Lazima tutoe lugha nzuri kwa wateja wetu”

5 September 2024, 12:08 am

Dr. Yusuph Steven Wambura, TMO Bunda (Picha na Edward Lucas)

Kaimu mganga mkuu halmashauri ya mji wa Bunda (TMO), Dr Yusuph Steven Wambura amewasisitiza watumishi idara ya afya kuhakikisha wanatoa lugha nzuri kwa wateja wanapofika kupata huduma

Amesema amekwisha ongea na watumishi na kuwaelekeza kuwa ” sasa hivi sio zamani zile mteja akifika kwenye huduma ya afya anatukanwa anaambiwa ulikuwa wapi, mbona umechelewa” kwani mtumishi yuko pale kwa ajili ya kutoa huduma

Sauti ya Dr. Yusuph S. Wambura

Dr Yusuph ameyasema hayo leo wakati akizungumza na radio Mazingira Fm ilipomtembelea na kufanya mahojiano naye kuhusu hatua mbalimbali wanazozifanya katika kusimamia na kuboresha huduma za afya

Aidha amesema watumishi wanaofanyakazi katika vituo vilivyo mbali na mji ni kweli wanachangamoto zao hivyo amesisitiza utaratibu wa kukaa na kusikiliza changamoto zao na kuzifanyia kazi

Sauti ya Dr. Yusuph S. Wambura