Mazingira FM

Mwanamke atoa mimba na kukitupa kiumbe kwenye shimo la choo

29 July 2024, 11:16 am

Baadhi ya viongozi wakikichukua kiumbe kwa ajili ya uchunguzi zaidi, Picha na Adelinus Banenwa

Mwanamke adaiwa kutoa mimba ya miezi saba na kukitupa kiumbe kwenye shimo la choo mjini Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Tukio limetokea July 29, 2024 mtaa wa Makumbusho kata ya Nyasura Halmashauri ya mji wa Bunda.

Mwenyekiti wa mtaa wa Makumbusho Ndugu Boniphase Musiba Mashenene amesema tukio hilo limetokea July 29 na baada ya kulipokea tayari muhusika anayedaiwa kutoa mimba hiyo amekamatwa na amekabidhiwa jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Eneo la shimo ambalo kiumbe hicho kilitupwa, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Mashenene amesema kama serikali ya mtaa wanakemea tukio hilo kwa kuwa linaharibu taswira ya mtaa na pindi wakiona hawana utayari wa kuzaa basi watumie njia zingine za uzazi wa mpango.

Sauti ya mwenyekiti Mashenene

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyasura Mhe Magigi Samweli Kiboko amesema matukio ya utupaji wa watoto na utoaji mimba yameonekana kushamili siku za hivi karibuni ameitaka jamii kuacha vitendo hivyo.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Makumbusho waliojitokeza kushuhudia tukio, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha amewata akina mama kama wanapata changamoto yoyote wakati wa ujauzito au wenye watoto wadogo watoe taarifa kwenye ofisi za ustawi au ofisi za serikali za mitaa.

Sauti ya diwani Kiboko