Mazingira FM

Mama adaiwa kutoa mimba na kutupa kiumbe kwenye pipa la taka Bunda

21 July 2024, 9:08 pm

Afisa wa Serikali akiwa amebeba kichanga kwa ajili ya uchunguzi zaidi, Picha na Godfrey Girani

Mwanamke mmoja ambaye hajajulikana, anadaiwa kutoa mimba inayokadiriwa kuwa na miezi mitano hadi sita na kisha kukitupa kiumbe hicho kwenye pipa la kutunzia taka

Na Mussa Kagole na Fadhil Mramba

Mwanamke mmoja ambaye hajajulikana, anadaiwa kutoa mimba inayokadiriwa kuwa na miezi mitano hadi sita na kisha kukitupa kiumbe hicho kwenye pipa la kutunzia taka kando kando ya barabara ya Mwanza Musoma eneo la stendi ya zamani halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara .

Sehemu ya Mapipa ya taka kilipokutwa kiumbe , Picha na Godfrey Girani

Akizungumza na redio Mazingira Fm msimamizi wa wazoa taka Sarah Philipo amesema alikuwa kwenye shughuli za utoaji taka kwenye kitunzia taka ndipo wakamuona mtoto huyo .

Kwa upande mwingine shuhuda wa tukio hilo Hamimu Issa amaesema tukio hilo limewasikitisha sana kwani ni jambo la kustaajabisha

Baadhi wananchi waliofika kushuhudia tukio, Picha na Godfrey Girani

Kagoye Mwenge ambaye ni Afisa Mtendaji Kata ya Bunda Mjini ni miongoni mwa viongozi waliofika katika tukio hilo na kuwaomba wanawake wanaojihusisha na matukio kama hayo kuacha mara moja kwani ni vitendo vya kikatili na vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara .

Sauti ya Kagoye Mwenge Afisa Mtendaji Bunda mjini