Mazingira FM

NMB yatoa msaada wa dawati 100 shule ya msingi Bigutu

29 May 2024, 6:51 pm

Viongozi wa NMB wakikabidhi dawati kwa mkuu wa wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

“wanafunzi hakikisheni mnayalina na kuyatunza madawati pia walimu hakikisheni mnayakarabati madawati yaliyoharibika” DC Naano

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano ameishukuru bank ya NMB kwa kutoa msaada wa madawati shule ya msingi Bigutu huku akiwataka wanafunzi kuyatunza madawati hayo.

Wanafunzi shule ya msingi Bigutu kwenye madawati yaliyotolewa na NMB Bank

Mhe Dkt Naano ameyasema hayo leo 29 May 2024 wakati akipokea msaada wa madawati kutoka bank ya NMB kwa shule ya msingi Bigutu iliyopo kata ya Bunda stoo halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara

Aidha  amewataka walimu wakuu wote wilayani Bunda na maafisa elimu ngazi ya kata kuhakikisha wanayakarabati madawati yote yaliyoharibika ili kupunguza changamoto ya watoto kukaa chini.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano, Picha na Adelinus Banenwa

Mhe Naano  amesema kwa wilaya ya Bunda kuna upungufu wa jumla ya madawati elfu 16 katika jumla ya shule 188.

diwani wa kata ya Bunda stoo Flaviani Chacha, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunda stoo Flaviani Chacha ameishukuru bank hiyo kuwa mdau wa karibu wa maendeleo huku akiwaomba wasiishie Bigutu tu bali waangalie namna ya kusaidia kwenye shule zingine.

Naye Dotto Makota kwa niaba ya meneja wa  NMB kanda ya ziwa, Picha na Adelinus Banenwa

Naye Dotto Makota kwa niaba ya meneja wa  NMB kanda ya ziwa amesema taasisis hiyo baada ya kupokea maombi walikubali kutokana na kwamba wao ni wadau wa maendeleo ambo wanasaidia  si katika elimu tu bali pia katika sekta zingine ikiwemo afya, na majanga mbalimbali.