Mazingira FM

Vijana washauriwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la akiba (mgambo)

24 May 2024, 12:06 pm

“Vijana jiungeni na mafunzo ya jeshi la akiba hakuna mateso bali zipo fursa “

Na Mariam Mramba

Imeelezwa kuwa wananchi kutokuwa na uelewa juu ya mafunzo ya jeshi la akiba na kutoshirikishwa katika mchakato wa kupata vijana wanaotakiwa kujiunga na jeshi hilo huwafanya wananchi kuwa na dhana potofu juu ya  mafunzo hayo.

Hayo yamebainishwa na wananchi wa kata ya Kabasa mtaa wa Nyasana katika mkutano ya hadhara ya utoaji wa elimu juu ya mafunzo ya jeshi la akiba.

Wananchi hao wamesema kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakitoroka nyumbani kwa kudhani mafunzo hayo ni mateso hali inayo sababisha wao kuogopa na kuzikimbia familia zao.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kabasa Mhe Selemani Joseph amewataka vijana wote wnye sifa za kwenda kwenye mafunzo ya mgambo kufanya hivyo kwa kuwa zipo fursa nyingi na mafunzo hayo siyo mateso.

sauti ya diwani