Mazingira FM

Ajinyonga chumbani kwake wivu wa mapenzi watajwa

1 April 2026, 10:09

Majirani hao wamesema jana majira ya saa mbili asubuhi walianza kusikia harufu kali ikitokea kwenye chumba hicho na nzi wengi ndipo walimpigia mwenye nyumba kisha kuwatarifu viongozi wa mtaa.

Na Adelinus Banenwa

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Amos Chacha 22 mkazi wa Kabarimu kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwenye chumba alichokuwa amepanga chanzo kikidaiwa kuwa wivu wa kimapenzi.

Majirani (wapangaji wenzake) wamesema mara ya mwisho waliona pilikapilika za kuwepo mtu kwenye chumba hicho tangu siku ya ijumaa ambapo wanataja walimuona mke wa kijana huyo akifungasha mizigo yake na kisha kuondoka huku kwenye chumba hicho akibaki kijana huyo akiwa anasikiliza mziki hadi majira ya jioni ambapo radio ilizimwa na tangu hapo hawakuona mtu tena.

Majirani hao wameongeza kuwa jana majira ya saa mbili asubuhi walianza kusikia harufu kali ikitokea kwenye chumba hicho na nzi wengi ndipo walimpigia mwenye nyumba kisha kuwatarifu viongozi wa mtaa.

Sauti ya Majirani (wapangaji wenzake)
baadhi ya wananchi wakishuhudia tukio la kijana kujinyonga

Felister Mama mzazi wa kijana huyo amesema mara ya mwisho alionana na kijana wake siku ya ijumaa akiwa na mke wake nyumbani kwake ambapo anataja kijana huyo alimtuhumu mke wake kwamba anamuibia vitu anapeleka kwao na baada ya kuwasuluhisha waliondoka kwenda wanapoishi

Mama hyuo ameongeza kuwa hakupata taarifa nyingine hadi pale jana alipopigiwa simu na mke wa kijana wake kwamba yeye aliondoka na yupo kwao kutokana na mume wake kumkataa mtoto, kabla ya leo kupata taarifa za mtoto wake kukutwa kwenye chumba chake akiwa amejinyonga

Sauti ya Felister Mama mzazi wa kijana

Kwa upande wake Kaimu mwenyekiti wa mtaa wa Kabarimu na balozi wa eneo hilo Victoria Joseph amesema amepata taarifa za tukio kwa wapangaji kuhusiana na sintofahamu ya harufu na nzi waliokuwa wakitokea kwenye chumba kimojawapo katika eneo hilo na baada ya kufika na kujilidhisha alichukua taratibu za kumpigia mtendaji wa kata na jeshi la polisi na baada ya kufika walivunja mlango ambao ulikuwa umefungwa kwa ndani na kukuta kijana huyo amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani aliyokuwa ameifunga kwenye kenchi.

Bi victoria amesema binafsi alikuwa hamfahamu kijana huyo na hajui ameamia lini ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wenye nyumba kuacha tabia ya kupangisha watu bila kutoa taarifa kwa viongozi na pia kwa wapangaji kuacha tabia ya kuingia kwenye nyumba bila kutoa taarifa ambapo kwa atakayebainika ni faini au kuondolewa kwenye mtaa.

Sauti ya Victoria Joseph makamu mwenyekiti