Mazingira FM

Afukiwa na kifusi akienda kutoa msaada mgodini

31 March 2026, 18:56

tukio hilo lilotekea tarehe 27/3/2026 majira ya saa kumi na moja jioni

Na Adelinus Banenwa na Mussa Kagole

Mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Nyamilama kata ya Kabasa alietambulika kwa jina la Mfungo Budigila 62 amefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi cha mchanga katika mgodi mdogo wa dhahabu uliopo  mtaa wa Nyasana kata ya Kabasa wilaya ya Bunda

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasana Amosi Mabula amesema tukio hilo lilotekea tarehe 27/3/2026 majira ya saa kumi na moja jioni ambapo mzee Mfungo wakati akiendelea na shughuli zake za kawaida jirani na mgodo huo ilisikia sauti ya mtu mmoja akiomba msaada kwenye shimo moja lilipo katika mgodi huo ndipo aliposogea kwenye shimo hilo lakini katika haraki za kutoa msaada aridhi ilimeguka na kumutupia ndani ya shimo hilo.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasana Amosi Mabula

Diwani wa kata ya Kabasa Daniel Yona amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha walikuwa wameshatoa maelekezo ya kufungwa kwa baadhi ya maduara ambayo yanaonesha hatari ya kuporomoka

Ametoa wito kwa wachimbaji na wananchi kuacha tabia ya kwenda kwenye maeneo ya mgodi huo ambayo yameshafungwa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza

Sauti ya Diwani wa kata ya Kabasa Daniel Yona

Awali moja ya mwanafamilia wa marehemu alisema tukio hilo wamelipokea kwa masikitiko makubwa na kwamba baada ya kupata taarifa ya ndugu yao kufukiwa na kifusi walikwenda moja kwa moja polisi ambapo baada ya kuhojiwa kuhusiana na kuridhika na chanzo cha tukio walikubali kwa kuwa mazingira yote yalionesha wazi kwamba ni ajali hivyo wamekabidhiwa mwili kwa ajili ya kuendelea na taratibu zingine za mazishi.

Sauti ya moja ya mwanafamilia wa marehemu