Mazingira FM

Mugeta wapewa kongole uandikisha wanafunzi

30 March 2026, 10:27

Mkuu wa wilaya ya Bunda, Mhe Aswege Enock Kaminyoge katika mkuno wa hadhara na wakazi wa kata ya mugetra Bunda DC kusikiliza na kutatua kero

Zaidi ya asilimia 96 ya watoto wanojiandikisha kuanza shule za msingi na sekondari wote wanafika shuleni.

Na Mariam Mramba

Mkuu wa wilaya ya Bunda, Mhe Aswege Enock Kaminyoge amewapongeza wananchi wa kata ya Mgeta kwa kufanikisha kwa kiwamgo kikubwa uandikishaji na mahudhurio ya wanafunzi ambapo zaidi ya asilimia 96 ya watoto wanojiandikisha kuanza shule za msingi na sekondari wamehakikisha wanafika shuleni.

Hayo amesama hivi karibuni alipokuwa akizungumza na wananchi hao ambapo DC Kaminyoge amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa kwani inaonesha uelewa mkubwa wa jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa maendeleo yawatoto na taifa kwa ujumla

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi hao kuendelea kushirikiana kwa karibu kuhakikisha wanafunzi hao wanapata chakula shuleni  ili kuwasaidia kuwa na afya njema, kuongeza umakini darasani na hatimaye kufanya vizuri katika masomo yao.

Baadhi ya wakazi wa mugeta waliojitokeza kumsikiliza mkuu wa wilaya katika mkutano

Kaminyoge ameainisha kuwa lishe bora ni msingi muhimu wa mafanikio ya kielemu na kuwahimiza wazazi kutekeleza jukumu hilo kikamilifu

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge